Hongerani mahafali, wakati umewadiya
Kweli Umetoka mbali, cheti ukakipokeya
Sasa unazo akili, za kuendesha duniya
Nakuhongera James, Siku yako Mahafali
Dunia yetu dunia, wasomi inawataka
Uirekebishe ndia, isije ikakutoka
Nakuombea Jalia,Ilahi Mola Rabuka
Nakuhongera James, siku yako mahafali
Nikiona cheti chako, hima moyo nafurahi
Ninajawa na chereko, masomo umeyawahi
Na hayapo masumbuko, zamani yaliyowahi
Nakuhongera James, siku yako mahafali
Yamekufika mengine, na ilaisha nguvu
Ukayaona manene, ila leo ni angavu
Na hata hao wengine, wanakuona mwangavu
Nakuhongera James, siku yako mahafali
Nakuombea kwa Mungu, uyapate yale mema
Yasikufike machungu, leo na hata daima
Ukiwa kwa ulimwengu, mazuri yaje waama
Nakuhongera James, siku yako mahafali
Wanjohi. P. Mugambi
Malenga Kitunguu Machoni

