John Rukono
Ni furaha yake mama, mwingi wa matumaini
Mateso yake waama, mwana nipate imani
Hakuiweka lawama, hata kiwa masikini
Furaha ya mama yangu, mwana ndiyo nilo nayo
Miezi tisa tumboni, mama liniangalia
Kwa uwezo wa Manani, mama akajifingua
Ni mdogo kwa yakini, na mambo sikuyajua
Furaha ya mama yangu, ndiyo mimi nilo nayo
Kijusi hadi kitoto, mamangu alinilea
Nikawa kama lipyoto, ila hakunichukia
Ningali bado mtoto, adabu linipatia
Furaha ya mama yangu, ndiyo mimi nilo nayo
Baba alienda zake, kumwacha mama mjane
Akalia asicheke, machozi yalo manene
Ila leo si makeke, aibu liisha tene
Furaha ya mama yangu, ndiyo mimi nilo nayo
Machozi huwa yatoka, kitaka usaindizi
Wana eti ni baraka, ila sivyo waziwazi
Mama naomba Rabuka, umkumbuke mzazi
Furaha ya mama yangu, ndiyo mimi nilo nayo
Bado mimi nipo shule, safari hini ni ndefu
Karo mama ipo tele, nakuomba Mtukufu
Lijaze hima wimbile, nisome japo marefu
Furaha ya mama yangu, ndiyo mimi nilo nayo
Yakini na taadhima, nitawa mvumilivu
Shule nitaweka hima, chudi ustahimilivu
Kesho nije kusimama, mamangu nami angavu
Furaha ya mama yangu, ndiyo mimi nilo nayo
John Rukono
Thika
Mwanagenzi- Giakanja Boys High School
Similar Posts by The Mt Kenya Times:
- Eldoret to host 2026 UN Tourism Week: Can the North Rift redefine Kenya’s tourism story?
- After Madrid chaos derby: Mourinho pulls out the printer
- Smart classroom revolution hits Nyeri schools
- Retirement is not a prison sentence: The Uhuru Kenyatta case and the defence of citizenship
- Taufiq Rafat: Voice of Pakistani English Literature