Joseph Okumu
Ya mambo pulikeni, masikizi andaeni
Kwa maozi tazameni, falisafa fairini
Yashangaza walakini, wanarika tuna nini
AI mwatumiaje, mbona zuri mwaharibu.
Kuna visa vyashangaza, vya kizazi cha kisasa
Jenzii wanabeza, viongozi kwa kukosa
Wawatia kwa jeneza, kichapisha kwa kurasa
Nayo X mwatumiaje, mbona zuri mwaharibu.
Mashababi na mabinti, TikiToku mefurika
Ya aibu wanaposti, wa nidhamu mepotoka
Kokeni mihadarati, wajifunza kulipuka
Jamani mwatumiaje, mbona zuri mwaharibu.
Kompyuta na rununu, mitandao inalipa
Teknolojia tunu, utafiti unajipa
Shule zetu pawe mbinu, tukasome yote hapa
Utandawazi hidaya, kiuchumi tunenepa.
Mtunzi: Joseph Okumu
Lakabu: Malenga Okumu
Kutoka: Busia, Budalang’i
Β©οΈ Poem Hunter 2025