Dr. Wanjohi. P Mugambi
Yaliza mpaka mfu, hali ya humu nchini
Kwa kuwa wale dhaifu, bado wasalia chini
Hata aliye kipofu, aona walo ta’bani
Hali ya humu nchini, yaliza mpaka mfu
Ukiwasikia hofu, yakujaa mtimani
Kiangalia marefu, wapatayo masikini
Ilhali majisifu, wajipa wa uongozini
Hali ya humu nchini, yaliza mpaka mfu
Huahidi maradufu, waingiapo bungeni
Wakakuwa maarufu, wakasahau jamani
Wakala mingi minofu, sambe kwanza hadharani
Hali ya humu nchini, yaliza mpaka mfu
Huwa wasahaulifu, kuwa sote tu ta’bani
Kwa wao uharibifu, tunalia abadani
Lini wata’cha machafu, heri wakatuauni?
Hali ya humu nchini, yaliza mpaka mfu
Yaliza mpaka mfu, hali ya humu nchini
Ila twaomba Raufu, atukinge maishani
Akatupe taarifu, tunapoenda debeni
Hali ya humu nchini, yaliza mpaka mfu
Dr. Wanjohi. PΒ Mugambi
Malenga Kitunguu Machoni
Similar Posts by The Mt Kenya Times:
- Mt Kenya Times ePAPER August 28, 2026
- Kenya is losing fifteen mothers a day β and the numbers are getting worse
- Consolata International University opens new academic year with call to humanise artificial intelligence
- Written in gold, wielded in iron: Katiba@16 and the realities of power
- Mang’eni challenges universities to put entrepreneurship at the heart of learning