Wanjohi. P. Mugambi
Vilio vilisikika, kwa wetu akina mama
Kotekote kadhalika, vidole wakaviuma
Wakajutia hakika, vifo vya wana waama
Giza lishika hatamu, kote na mote nchini
Wengi wakalaza damu, wakaenda vidandani
Kukakucha nayo sumu, Edarasha i motoni
Wazazi tokea kote, walishika zao njia
Shuleni wafike wote, hakika kushuhudia
Ila waloona chote, machozi liwajazia
Walikuwa mahututi, na wengine marehemu
Za wanafunzi sauti, peponi zililazimu
Ikawa ni harakati, watambulike jukumu
Machozi waliyalia, wazazi wakiduwaa
Moto umewachukua, wanao wa manufaa
Nguvu zikawaishia, wakabaki kunyamaa
Habari na vidokezo, zilipas runingani
Na sababu mzomzo, kuteketea kwa bweni
Kila mtu lake wazo, hata wale wongozini
Ulifikia wasaa, rais akasimama
Akaiita balaa, kina baba kina mama
Kawatakia hewaa, iwatulie mitima
Aliamrisha tume, kuuchunguza mkasa
Ili mioto ikome, shule zipigwe msasa
Ila bado ni kinyume, yaongezeka mikasa
Kwazo zote familia, ipokeeni
Makiwa
Wale walotangulia, msalimuni Moliwa
Ndiyo yetu sote njia, japo chanzo sio sawa
Wanjohi. P. Mugambi
Malenga Kitunguu Machoni
Similar Posts by The Mt Kenya Times:
- Classrooms for Kenya boosts learning infrastructure at Bikeke Junior School in Trans-Nzoia County
- Former Mau Mau fighters mourn Githui Karue, hail him as champion of freedom and culture
- Data over collateral: Why digital transactions are the future of informal credit
- PSV Saccos urged to deepen savings and financial skills to drive sustainable growth
- Mt Kenya Times ePAPER July 25-26, 2026