Mugo Romeo Wachira
By: Wanjohi. P. Mugambi
- Hebu tueleze mengi kukuhusu.
Kwa majina yangu nafahamika kama Wachira Romeo Mugo (MORIO) nilizaliwa tarehe 3/1/2007 Kata ndogo ya Tinderet eneo mbuge la Tinderet kaunti ya Nandi. Mmi ni wa pili katika familia ya wana watano. Wazazi wangu ni bwana Joseph Wachira na Bi. Catherine Nyambura. Masomo yangu yaling’oa nanga 2011 shule ya chekechea na nikasoma mwaka mmoja tu kwa sababu nilikuwa mweledi. Baadaye nikajiunga na shule ya msingi wa Tinderet mpaka darasa na nne, baadaye nikajiunga na shule ya kibinafsi la harmony hadi darasa la sita.kwa sababu tulikoishi kaunti ya Nandi ilikuwa shughuli za kikazi ilibidi tuhamie na mamangu mzazi kaunti ya nyandarua tunakoishi sasa. Nikajiunga na shule ya msingi ya kahuho iliyoko Nakuru Eneo bunge la Gilgil nilikokamilisha masomo yangu ya shule ya msingi na kujizolea alama 332. Kwa bahati mbya au nzuri sikupata barua lolote la shule ya upili jambo lililonikera kwani ndoto yangu ya kujiunga na shule ya kitaifa ya Kapsabet ilizimwa
Kwa sababu babangu mzazi alikuwa bado kaunti ya Nandi akaniarifu kuhusu shule ya upili ya st John’s Tachasis ilivyokuwa inanawiri. Sikuwa na budi ila kujiunga na shule hiyo ambayo ilinifunza mambo mengi zaidii Kiswahili kikiwa na hadhi ya juu zaidii kwa sababu ya utangamano na wanafunzi kutoka makabila tofauti. Nilizidi kupambana Kila kuchao ili ndoto zangu zikuwe ni za kutimia siku moja
Nilifanikiwa kusoma hadi kidato cha Nne na nikaufanya mtihani wangu wa kitaifa 2023 nikiwa na mwingi wa matarajio kwa sababu za bidii za mchwa nilizozifanya. Hatimaye ulichokipanda ni lazimaa uvune matokeo yalipotokea nikawa na alama ya B ambayo kwangu halikunifurahisha Zaidi kwa sababu azma ilikuwa A- ili niweze kufanya uanasheria kuwa sikuwa na lingine ila kumshukuru mola kwa maana yeye ndo mpaji na linijua kuwa ana sababu. Mwaka 2024 nilifanikiwa kujiunga na chuo Kikuu cha Murang’a kama mwanafunzii anayepania kuwa mwalimu wa Kiswahili na historia .Kazi yangu ya kubuni mashairi na kughani ilianzia kule shule ya upili ambapo nilikuwa na ushirikiano mzuri kati ya walimu wa Kiswahili. Kwa hakika nilikuwa nakipenda kiswahili Kila mara tukiwa na mkutano au gwaride ungenisikia nikighani mbele ya wanafunzi wenzangu ambapo nilikuwa malenga tajika na hapo ndipo lakabu MORIO lilitokea. Walimu walizidi kunipa morali bwana Mulama, Barasa na Asiema na Bi. Tormoi kwamba siku moja nitakuja kutimiza lengo langu la uchapishaji wa mashairi na kuandika vitabu. Nilipojiunga na chuo kikuu cha Murang’a hata sikukawia wiki kama sijajiunga na CHAKIMUT kinachokuza vipaji na Kiswahili kwa jumla. Hapo ndipo nilipatana na Raphael tuju, Sam mungai , Japheth na Ustadhi Karma walionitia nguvu kwa mkutano uliofanikishwa na Vincent Mutunga
Kutoka hapo nimekuwa nikitunga mashairi kila kuchao na kutumia watu binafsi na pia taifa leo japo sjawai pata nafasi ya kuchapishwa ila nina matumaini Zaidi kwani wakati wa mungu ukifika hakuna kupinga.
- Ni nini kilikuchochea hasa katika tasnia hii.
Kwa kweliii Kiswahili nilikianza kukisikiliza utotoni kupitia redio maisha katika kipindi cha Jumamosi ilikuwa lazimaa kama ibada nyumbani kwetu kusikiliza kipindi hicho kwanii usipofanya hivyo ungeona cha mtema kuni. Waandishi waliobobea kama Guru Wallah bin Wallah, Ken Walibora mara nyingii walipenda kuja studioni jambo hilo lilinifanya kujua zaidii Kiswahili. Siku moja nikiwa kidato cha pili nikawa wa kuenda kwenye shule ya kitaifa moja na nikapatana na malenga aliyeghani shairi lililonifurahisha zaidii na ikanitia nguvu zaidi nikaanza papo hapo safari ya utunzi wa mashairi pia. Kwa hakika nilifanikiwa kwa sababu nilipoenda kongamano la vijana kaunti ya Nandi niliibuka mshindi kwa kumghania kiongozi Allan Kosgei shairi zuri sana. Nuru bakari pia ni mtu ambaye hunipa furaha siku zote na natumai siku moja nitakuwa kama yeye
- Siku yako huwa vipi kunapokucha.
Mmi huamka asubuhi ya 5:40 kwa sababu ya maombi na kusoma bibilia jinsi tunavyotakiwa na kozi ninayoifanya ya CBR (Consistent bible reading) baada ya hayo ninapanga mradi wa siku kwanza kama nina darasa nikaingie kisha nikiwa shuleni nikaangalie gazeti nisome. Usafi wa nyumba kama kawaida na kuandika kama ni shairi, kusikiliza muziki pia napenda zaidii, kisha jioni mara nyingii nina shughuli za kanisa lazimaa nikaende. Jambo jingine ni zoezi la mwili na kucheza mpira ni mara mbili kwa wiki.
- Ni kipi kinakupendeza katika kazi yako?
Zaidii kinachonipendeza ni kuona nikiangaza kwa vile mashairi zangu huzituma katika mitandao za kijamii .Watu wakizifurahia na kunipongeza zaidii lanitia moyo zaidii .Pia kuwajumuisha wenzangu kama lewis ,Carlos na wengineo nimechukua hatua ya kuanza kuwalea na kuwaonyesha mikakati na njia mwafaka pia wao watimize zao ndoto.Pia kutumia mashairi kuendeleza neno la mungu jambo Hilo lanipendeza pia zaidii
- Ni kitu kipi kigumu kwa yale unayofanya.
Jambo gumu kwa uandishi mara nyingii ni muda .unapata unatamani zaidii kuandika kazi yako kwa upana ila muda hairuhusu wakati mwiingine mmi najipata Nina shughuli nyingii na inanibidi nijitenge kidogo na kazi yangu kwa muda fulani.Jambo la muda mara nyingii husumbua kwani kutoa kazi nzuri yataka muda mzuri na mawazo yako, na pia yaitaji ubunifu wa Hali ya juu zaidi kuwa mshairi yataka uwe mtu wa kufikiria zaidi kwani matukio yanafuatana sana na inakubidi uweze kuwa wa haraka kujuana na mazingira ya matukio.
- Umewahi kupata changamoto katika kazi yako? Tuambie kuihusu.
Changamoto kubwa iliyonipata ni niliposema nataka kufanya kiswahili na historia chuo kikuu lillikuwa jambo ngumu kwa wazazi na wanakijiji kwa sababu ya dhana potovu walikuwa wananilazimu niwe mwalimu wa hesabu lakini nikasema liwe liwalo.changamoto nyingine ni kuwa unaandika mashairi mengi ila mahali pa kupeleka ndo unakosa kwa sababu ya changamoto za hela za kuchapisha diwani. Pia mara nyingi taifa leo huwa na ushindani tunatatuma lakini hazichapishwi jambo hilo linaweza kufanya ufe moyo kwa kiasi kubwa lakini natumai ipo siku
- Ni kipi kinachokusaidia kupambana na changamoto hizo?
Kwa kuchapisha diwani,tuna miradi na wenzangu wa kuchanga hela Kisha tuweze kuchapisha diwani moja baada ya nyingine ili kupunguza gharama za kuchapisha na pia kutiana moyo kama CHAKIMUT.Pia mmi ni mtu ambaye Nina roho mgumu wa kufa moyo huwa naamini nitapambana mpaka mwisho na kuna siku nitafanikiwa.Pia kumcha mungu na kumwaminia na kuiombea kazi yangu Kila kuchao ni mikakati moja wapo ambayo nimeiweka mbele
- Huwa unatangaza kazi zako? Tuambie hatua unayoitumia.
Mimi hutangaza kazi yangu kwa mitandao za kijamii kama Facebook na haswa kwa vikundi mbali mbali ya wasapu kiwemo waandishi wa Afrika na vikundi vingi vya Kiswahili chuoni na hata CHAKITA, Pia tukiwa darasani na mikutano mingi mmi hupatana na wanafunzi na kuweza kuwapa kazi zangu na tunapena mawaidha. Isitoshe, huwa nawaandikia na kuwaghania mashairi jambo ambalo wakati mwingi hunipa hela ya kuweza kujimudu kwa maisha ya kila siku. Natumai hivi karibuni nitafungua akaunti nyingi na kupata kuitangaza kazi yangu ili niweze kujikuza zaidi
9 Kwa yule ambaye anatamani kupata kazi zako atazipataje?
Kwa yeyote Angependa kuona kazi yangu anaweza kuwasiliana nami kwenye nambari 0794729779 wasapu na tiktok @malenga mugo Romeo.Facebook Romeo Wachira au mugowachira229@gmail.com kwenye barua pepe na ataweza kunipata