Zimepita siku nyingi, hili niliseme wazi
Hakika ni muda mwingi, naliamba waziwazi
Umepita mambo mingi, kufika kwa hini ngazi
Nakupongeza Kimani, siku yako kuhafali
Umepigana na kazi, ulipoingia chuo
Ukasikiza walezi, ufikie chako cheo
Leo wavaa mavazi, chako chetu nacho chao
Nakupongeza Kimani, siku yako kuhafali
Nikuonapo nakiri, naona binti mahiri
Aliyeionja shari, kugeuza kuwa shwari
Leo twaiona heri, hongera kweli nakiri
Nakupongeza Kimani, siku yako kuhafali
Ni mengi umeyaona, ukitimiza maono
Ila yote ni bayana, yako wewe mapambano
Hivyo hongera nasema, zifike kokote kuno
Ninakupongeza Kimani, siku yako kuhafali
Nionapo nafurahi, bila kinyongo moyoni
Kwayo yako nimewahi, kukushika mkononi
Nawe wani umewahi, leo sote furahini
Ninakupongeza Kimani, siku yako kuhafali
Imejia siku yako, ukaweza kuhafali
Ujawe nazo chereko, kwayo uliyokabili
Na wazazi furahiko, kwa mengi mema kikweli
Ninakupongeza Kimani, siku yako kuhafali
Nitazidi kukusifu, wasikie duniani
Kwani sitokukashifu, huna ovu hata wani
Nitaandika wasifu, wakujue abadani
Ninakupongeza Kimani, siku yako kuhafali
Zidi na uzidi sana, ufikie kileleni
Shahada nyingine tena, ujipatie yakini
Na usipotoke mwana, mazuri uzidisheni
Ninakupongeza Kimani, siku yako kuhafali
Lililo zuri shairi, kiujuzi namaliza
Wakutambue mahari, mwendo umemaliza
Ila ukajue mwari, ndo mwanzo unaangaza
Ninakupongeza Kimani, siku yako kuhafali
Wanjohi. P. Mugambi
Malenga Kitunguu Machoni
Similar Posts by The Mt Kenya Times:
- Africa reels from energy shocks, Ebola fears and growth slowdown as Middle East conflict ripples across continent
- Argentina beat Algeria 3-0 in World Cup clash as Messi nets hat-trick
- France defeat Senegal 3-1 as Mbappé double fires Les Bleus to victory
- Accounts committee probes audit queries on office of the President accounts
- Kenya hunts new coffee markets