HEKO ESHIKULU
Nalitunga langu tungo, na maneno mateule
Na sera zenye kiwango, pamoja tusonge mbele
Njongeeni kwenye jengo, niwajaze mambo tele
Kwa hichi nawapongeza, wasomi wa Eshikulu
Masomo mumeyakuza, chipukizi na bobea
Hekima mkaijaza, na wengi mkaelea
Nyote ninawapongeza, kama Omayio pia
Kwa hichi nawapongeza, wasomi wa Eshikulu
Kuwataja sitoweza, wasomi wa Eshikulu
Kwani nyote mmeweza, kutupa ya zuri lulu
Twafurahi kuangaza, kwa vile mumefaulu
Kwa hichi nawapongeza, wasomi wa Eshikulu
Zangu beti namaliza, zilizojaa wasifu
Nikiomba miujiza, mjaliwe maradufu
Na guu mkajikaza, maisha yawe ya nuru
Kwa hichi nawapongeza, wasomi wa Eshikulu
Dan Wanambisi
Mwalimu Dawa
Kakamega
Similar Posts by The Mt Kenya Times:
- Communities secure historic land rights as Wahome issues 60 title deeds across 369,000 acres in Samburu
- Ahadi Kenya Trust closes chapter on jigger campaign with historic archive
- Antony Gitonga Foundation to hold free medical camp in Othaya
- Mt Kenya Times ePAPER May 28, 2026
- Sinner storms into Roland Garros second round