Wanjohi. P. Mugambi

Moyo wangu ni hafifu, haya ninapoyanena

Una mengi masumbufu, jinsi yalivyo bayana

Unatariki mapafu, kiyawaza kwa mapana

Wawaza mambo ya penzi,  penzi lilousaliti

 

Ulipendwa kiukweli, kama hungependa tena

Ungafunguka asali, ikawa ndo mlo sana

Ila umeonja ukali, nayo makali wavuna

Wawaza mambo ya penzi,  penzi lilousaliti

 

Ni mnyonge huu moyo, yakini nguvu hauna

Na yote uyawazayo, majibu yake hauna

Kwa penzi lenye uchoyo, wavunja damu kwa kina

Wawaza mambo ya penzi,  penzi lilousaliti

 

Unatamani ya wafu, duniani waso nena

Kwani heri kuwa mfu, ya duniani mepona

Kuliko ya ubarafu, penzini unaovuna

Wawaza mambo ya penzi,  penzi liloisaliti

 

Mtima unasumbuka, kwa marefu na mapana

Unatamani hakika, na dunia kuachana

Uchunguni ukatoka, tulio lenye maana

Wawaza mambo ya penzi,  penzi lilousaliti

 

 

Wanjohi. P. Mugambi

Malenga Kitunguu Machoni

Nairobi Kenya

Similar Posts by Mt Kenya Times:

By The Mount Kenya Times

We are The Mount Kenya Times. For customer care, 📨 info@mountkenyatimes.co.ke or 📞 +254700161866 For feedback to editorial, 📨 news@mountkenyatimes.co.ke or 📞 +254705215262 or WhatsApp +254714090155

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *