Mwalimu Wanjama Frank
Mama ee! Mama ee! , twakulilia mametu
Hasira tupunguzie , twajuta nafsi zetu Jongea tukulilie , okoa maisha yetu
Janga hili mafuriko , ni mwiba wa kujidunga
Bukurata wa ashiya , mama uaraukia
Jasho lako lakupwaya , kiononi kafungia
Mifereji funguliya , ya mbinguni na duniani
Janga hili mafuriko ni mwiba wa kujidunga
Mabwawa yote e maama, pomoni uliyajaza
Mabonde hata milima , mafuriko yatatiza
Kitafuta usalama , gharika yakufukuza
Janga hili mafuriko ni mwiba wakujidunga
Mwaka juzi ni solai , kukawa kilio tele
Kafuata jitimai, mahi mahiu fikile
Dakika kupiga chai, hamkuwa cha simile
Janga hili mafuriko ni mwiba wakujitakia
Misitu tulivamia ,kaharibu maumbile
Viwanda moshi hutoa , angani yachafukile
Taka zote tukitoa ,kiholela twatupile
Janga hili mafuriko ni mwiba wakujidunga
Naye mama maumbile , msamaha ni adimu
Hasira zake ni tele, sikia hili muhimu
Zitaangamiza ndwele , mafuriko yakidumu
Janga hili mafuriko ni mwiba wa kujidunga
Tumtole tambiko , mametu hapo alipo
Hebu akae kitako , Baraka azitowapo
Tusimpe maudhiko, epuka chake kichapo
Janga hili mafuriko ni mwiba wa kujidunga
Tukiacha kemikali , za kudhuru mazingira
Na tutii serikali , sharia zake imara
Ukitii una kinga , mafuriko yakibisha
Janga hili mafuriko ni mwiba wa kujidunga
Hapo natia nanga , beti kenda zinatosha
Hizi lulu mezipanga , ujumbe nimewapasha
Ukitii una kinga , mafuriko yakibisha
Janga hili mafuriko ni mwiba wa kujidunga
MTUNZI; Mwalimu Wanjama Frank
SIMU; 0721609433
BARUA PEPE; wanjamafrank@gmail.com
MAHALI; Mwalimu, shule ya upili ya Ihithe eneo bunge la Tetu ,Gatuzi la Nyeri
Similar Posts by The Mt Kenya Times:
- Mt Kenya Times ePAPER August 28, 2026
- Kenya is losing fifteen mothers a day — and the numbers are getting worse
- Consolata International University opens new academic year with call to humanise artificial intelligence
- Written in gold, wielded in iron: Katiba@16 and the realities of power
- Mang’eni challenges universities to put entrepreneurship at the heart of learning