Brian Oigara
Nisije kwenye mazishi, nikalia kikwikwikwi,
Nikijifanya mbishi,lawama ni kwa ukukwi,
Wetu mterehemeshi,aki ya Mungu hazikwi,
Pepa Lobawoi pepa, maua yako nakupa.
Nisije nikajifanya,kuwa mwingi wa subira,
Kivyovyote kujikanya, ningoje mambo kubura,
Mashabiki ukisanya, ndiposa nikupe kura,
Pepa Lobawoi pepa, maua yako nakupa.
Chema nakiitwe chema, watu wote wasikie,
Wewe ni rafiki mwema,naomba nikisifie,
Mola akupee neema, ya kheri akujalie,
Pepa Lobawoi pepa, maua yako nakupa.
Tungetamani dunia, yenye watu kama wewe,
Watu wasio udhia, wanyofu waso kiwewe,
Kwa kweli tungetulia, na kupendana wenyewe,
Pepa Lobawoi pepa, maua yako nakupa.
Mwisho wangu ndio huu, bingwa uzidi kutamba,
Ufike na huko juu,ntini upawe namba,
Magazeti yanukuu, hoja zako ukiamba,
Pepa Lobawoi pepa,maua yako nakupa.
Brian Oigara
Malenga Mla Leo
Similar Posts by The Mt Kenya Times:
- Dr Rania Lampou: The woman who turned a classroom into the world
- The Darkness Within: A Critical Review of Joseph Conrad’s Heart of Darkness
- Diaspora Times Global Sep 5 – Sep 11, 2026
- Mt Kenya Times ePAPER September 5-6, 2026
- Kenya secures AGOA extension to 2028, unlocking continued duty-free access to US market
Kazi aula hii Be. Wanjohi. Napendezwa na Gazeti hili kwa kunyanyua vipaji.