Tahakiki ya Tamthilia “KIMYA” kilichoandikwa na Said .A.Mohammed

Kitabu: KIMYA
Mchapishaji:Longhorn
Kurasa:94
Mhakiki: Winjoy
KIMYA ni tamthilia iliyoandikwa na Said .A.Muhammed.Tamthilia hii Ina wahusika wafuatao;Be.Binafsi,Bi.shoo,Mpya,Mussa,Zanga,Be.Naona,Be.salimina,Bw.Taja,Bi.Mgeni,Be sikilivu,Bi.subira,Mpishi,Fumbo,kushoto,Kulia,wananchi,Mkemeo,Sauti,Sauti ya ndani kisimani,sauti ya mpya,sauti ya too,sauti ya Umma.
Kimya ni tamthilia inayoshughulikia masuala ya kijamii na kiuchumi katika jamii za kisasa.Tamthilia hii inalenga kuonyesha athari za Kimya katika maisha ya watu.Tamthilia hii inachambua jinsi Kimya kinavyoweza kuwa na maana tofauti katika mazingira mbalimbaliTunapata mvutano baina ya kulia na kushoto umekua mzito.Mbele hawaendi nyuma hawaendi kulia na kushoto hawaendi kushoto anataka kwenda kulia hawezi Kulia anataka kwenda kushoto naye hawezi pia.Kwa kuelekezana migongo na kuvutana pande zote hawaendi popote.kushoto analalama mbona haendi mbele anajitahidi anajivuta anajisukuma lakini…”kumbe sababu yote ya hay ni Kimya! Hali hii itabadilika pale tu watakapokaa Kimya na wakiruhusu Kimya kusema mpaka pale mdogo atamfundiaha makubwa kusema pole.Mpaka pale ulimi uliogada kwenye Baraza na kitasena Kimya kinya Kwa sauti kubwa ya yoo.
Ningependekeza kitabu hiki kisomwe na Kila mmoja anayependa kujifunza.Hadithi Kwa hii tamthilia zinafanyika katika mji mdogo ambapo wahusika wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama Njaa na umaskini.Tunapata ja anatokea kushoto ya msitu anaitwa kushoto na mwingine anatokea kulia ya msitu anaitwa kulia.Wote tunaambiwa wanajitimai na hofu ya kupoteza tunapata kuwa njaa ya miaka imewabana,Kiu ya karme inawaatilisha ambapo wanakutana kwenye kisiwa kikavu Cha maji yasiyotekeka.Tamthilia hii inachunguza uhusiano na wengine na jinsi jamii inavyojibu matatizo ya wahusika.
Saidi .A.Mohammed mwadishi wa hii tamthilia anatumia mtindo wa kuandika ambapo unasisitiza mazungumzo na mwingiliano wa wahusika.Lugha anayotumia ni rahisi na ya kueleweka huku ikichamgamua hisia za huzuni na matumaini.Maelezo ya wahusika na mazingira Yao yanaweza kumfanya msomaji ajihisi kama sehemu ya hadithi.Mhusika kulia tunapata anasema ama kweli hiki ni kizungumkuti maana anataka kuenda kushoto lakini Kwa sababu fulani inaningangamiza kulia.Anazuiliwa hapohapo kulia kifikra.Anasema utandawazi unataka abaki hapohapo ambapo anasema walijisukumiza kulia tokea mawazo.Hili linatupata sisi binadamu ambapo hatujui twende na wapi mara nyingine.
Tamthilia hii inatoa ujumbe mzito kuhusu umuhimu wa sauti na Mawasiliano katika jamii.Kitabu hiki kinasisitiza kwamba Kimya hakijakosekana maana,lakini kinaweza kuleta madharau makubwa .Kimya pia kinachangiza wasomaji wafikilie kuhusu umuhimu wa kuzungumza na kutafuta suluhu Kwa matatizo yanayowakaba. Tunapata Mhusika mmoja Kwa Jina mpya anasema amechoka kusubiri.Amechoka kungojea,kunyamaza anasema huku kunyamaza ndiko kunakomwangamiza na wote nchini.
Kwa Hitimisho naeza sema kuwa tamthilia KIMYA ni tamthilia yenye nguvu inayowasilisha masuala ya kijamii Kwa njia ya kuvutia mno.Inatoa mwanga juu ya changamoto za maisha ya Kila siku na umuhimu wa Mawasiliano.Katika kutatua matatizo .Ni kazi inayofaa kusomwa na yeyote ili kuelewa masuala ya kijamii.Kupitia tamthilia hii naeza sema kuwa said.A.Muhammed alikua anaionea jamii ya kesho na Leo na kuitabiria yatakayoisibu

