Fatma Ali Mohamed
Mimi mti wa jangwani, ukame nauhimili
Hata nitupwe jaani, haifi yangu asili
Watu wananithamini, japo kuwa bei ghali
Uzuri wangu wa tende, utamu wa kuzaliwa
Tofauti na makande, sukari yanayotiwa
Haluwa vipi ishinde, utamu wa kughushiwa
Hawatoniweza tende, mimi nimejaaliwa
Uzuri wangu wa tende, utamu wa kuzaliwa
Tende ninapendwa sana, na watu wa rika zote
Ninapoadimikana, ninatafutwa popote
Wanaranda Kila kona, ladha yangu waipate
Uzuri wangu wa tende, utamu wa kuzaliwa
Mtunzi: Fatma Ali Mohamed
Mahali: Pemba
Similar Posts by The Mt Kenya Times:
- Written in gold, wielded in iron: Katiba@16 and the realities of power
- Mang’eni challenges universities to put entrepreneurship at the heart of learning
- Why Jetour struggles to build a fan base in Kenya
- Spleng School Ruiru students enjoy an exciting educational trip to Malindi
- The three-legged stool is wobbling