Joseph Abuko
Afrika bara zuri, tuna vingi vyapendeza,
Tunavipaji vizuri, vyenyewe vyajitangaza,
Michezoni tu pazuri, na kandanda tunacheza,
Afrika tunavingi, vizuri twajivunia.
Madini tumejaliwa, dhahabu na almasi,
Hakika tulizaliwa, kwenye Bara zuri sisi,
Afrika mambo sawa, tunalindwa na polisi,
Afrika tunavingi, vizuri twajivunia.
Tuna miti tofauti, kweli madhari mazuri,
Miti inaunda kiti, chapendeza ni kizuri,
Na wanetu mabanati, wanapendeza wazuri,
Afrika tunavingi, vizuri twajivunia.
Tunapenda tamaduni, kuanzia kwa mavazi,
Tunavalia vipini, urembo wetu u wazi,
Na tunalima shambani, sisi ni wachapakazi,
Afrika tunavingi, vizuri twajivunia.
Na tamati nimefika, tuipende Afrika,
Ni Bara nzuri hakika, bara lenye uhakika,
Na Vyakula vya kupika, vipo vipo Afrika,
Afrika tunavingi, vizuri twajivunia.
Mtunzi: Joseph Abuko
(Chuo Cha ICS Nakuru)
Similar Posts by The Mt Kenya Times:
- Consolata International University opens new academic year with call to humanise artificial intelligence
- Written in gold, wielded in iron: Katiba@16 and the realities of power
- Mang’eni challenges universities to put entrepreneurship at the heart of learning
- Why Jetour struggles to build a fan base in Kenya
- Spleng School Ruiru students enjoy an exciting educational trip to Malindi