MOMANYI HENRY RIOBA
Wan’fuu nawatungia, la kheri kuwatakia
Siku zimekaribia, mitihani imewadia,
Ngariba anaingia, kwa njia ya kuvizia,
Wanafuu nawatungia, la kheri kuwatakia
Kwa muda mmesubiri, wakati huu kufika
Mlipo muwe jasiri, tena msije tishika
Pumuzika kwa kadiri, punguza nayo mashaka
Wanafuu nawatungia, kila la kheri kuwatakia
Msije kuchacharika, kwa uvumi usofaa
Wengi wapenda mashaka, kusudi kuwahadaa
Mtegemee rabuka, kwa yote atakufaa
Wanafuu nawatungia, la kheri kuwatakia
Mitihani ile ile, aghalabu mmefanya
‘Soni la kuleta ndwele, muwanze kubambanya
Yatoe majibu tele, Wala yasiyokanganya
Wanafuu nawatungia, kila la kheri kuwatakia
Maagizo aghalabu, uyasome sawasawa
Muhimu nayo adabu, siku zote uwe sawa
Vyote ni Kama dhahabu, kwako kuwa maridhawa
Wanafuu nawatungia, kila la kheri kuwatakia
Beti sita ndizo zenu, kalamu naweka chini
Zitimie ndoto zenu, ‘livyopanga aushini
Zijibiwe dua zenu, ‘takavyopenda manani
Wanafuu nawatungia, kila la kheri kuwatakia
MTUNZI: MOMANYI HENRY RIOBA
LAKABU: MALENGA MTANASHATI
ENEO: KESOGON