By STEVE DEFIANT ONDIRE.
Nilikuwa na mpenzi wangu ambaye sisi sote tulitarajia atakuwa MKE WANGU. Nilipojiunga na chuo kikuu, mpezi wangu alinionya niepukane na SAMAKI WA NCHI ZA JOTO. SHAKA YA MAMBO. Ajabu nikuwa, baada ya miaka mitatu, Mapenzi yakawa GILASI YA MWISHO MAKABURINI! Laiti ningalijua kwamba Haya yote yalikuwa tu NDOA YA SAMANI!! Ajabu ni kwamba, alinisinzia kuwa ninaye Mtoto nje ya mapenzi. Swali langu hadi wa leo ni; Yuwapi huyu MWANA WA DARUBINI? Baada ya kuvunjika kwa mwiko, maisha ikawa KIKAZA siku nenda siku rudi. Hatimaye nikampenda malaika Mwingine. Kama kawa, hapa pia tukapitia MAEKO. Nilimpenda kwa dhati. Nikamjali na kumuenzi sana. Mapenzi yakawa sambamba. Lakini sintofahamu zilipotokea, lawama nikarushiwa zote. Mzigo Huu ukawa KANDA LA USUFI!
TULIPOKUTANA TENA na mpenzi wa zamani, niliapa siyataki tena MAPENZI YA KIFAURONGO.
Mwenzenu mie kazaliwa na hayati MASKINI BABU YANGU. Maishani mwangu tangu utotoni, nimekuwa niki- TAZAMANA NA MAUTI si njaa, si Karo, si ajali barabarani, si kuvamiwa na wakora, si magonjwa sugu, si maradhi ya moyo, nakadhalika. Licha ya hayo, Nina NDOTO YA MASHAKA yakwamba ingawa ninalo DAMU NYEUSI, na kubeba TUMBO LISILOSHIBA, nitapambana na MASHARTI YA KISASA Liwe liwalo! MWALIMU MSTAAFU aliniambia hakika kabla uheshimike na kuitwa MKUBWA, ni lazima uwe umeyafuzu MTIHANI WA MAISHA. Nami hapa nitamenyana na kujikaza Kama KIDEGE nikiwa na imani kwamba MIZIZI NA MATAWI zangu zitafanya ning’ae, na nipige SHEREHE. Ajabu ya Waafrika, Mungu akitubariki tule tushibe, na tena SHIBE INATUMALIZA.
NIZIKENI PAPA HAPA nitakapowaaga.
Similar Posts by The Mt Kenya Times:
- Opposition will have a candidate by April, says Gachagua
- Kalonzo takes his campaign to the people across three counties
- Kenya’s election technology tender: A KSh10B procurement under fire
- The goon question: What Ruto’s vow to act personally really means for Kenya
- Kindiki: Common African standards are the key to Africa’s $3.4 trillion market