Cornelius Nasong'o Wafula
Cornelius Nasong’o ni mwanahabari kitaaluma.
Amejikita katika makuzi ya lugha ya Kiswahili na kuviendesha vipindi kadha wa kadha mathalan msingi wa Kiswahili kama nahodha msaidizi (NIBS FM) Miale ya Spoti na hata kuchangia magazetini ; Gazeti la taifa leo kwenye mjadala na barua kwa mhariri, kisha gazeti la MT. KENYA TIMES ambapo anayaandika makala ya Spoti.
Maishani Kuna Siri
Hii dunia duara, tuishi
kiajuadi,
Tusijitie papara, pia hata makurubundi,
Tukumbatie shajara, maisha bora kusudi,
Maishani kuna siri, tuishi kwa ubaraza.
Tupunguzeni hasira, hawa waja wana tadi,
Kupunguza kudorora, maisha yatufanidi,
Tuukabili uchwara, pasipo na uhasidi,
Maishani kuna Siri, tuishi kwa ubaraza.
Tukiwa kwenye hadhara, tufaane kwa ahadi,
Tujinasue kwa mara, maisha hayana budi,
Na uishipo msira, kesho fumbo jiadidi,
Maishani kuna siri, tuishi kwa ubaraza.
Dunia ina ujira, jichunge na usawidi,
Utaitibua dira, matukio ya kijadi,
Tuinjike subira, pamoja na usafidi,
Maishani kuna siri, tuishi kwa ubaraza.
Mtunzi: Cornelius Nasong’o
Lakabu: Askofu wa soka