Wanjohi. P. Mugambi

Wanjohi. P. Mugambi

Malenga Kitunguu Machoni

Nairobi Kenya

Mwambie nilipo leo,  si pale nilipokuwa

Yamegeuka ya leo, mengine yameshakuwa

Sicho kile kichocheo, mtima kilichouwa

Mwambie!

 

Mwambie letu eneo, si hivyo lilivyokuwa

Leo linao noleo, lanoa bongo visawa

Hakuna mapendeleo, jinsi yalivyokuwa

Mwambie!

 

Mwambie nilipo leo, kwake nipofukuziwa

Mwana lipata pepeo, faudi kutuliziwa

Nitatulia tokeo, mi’ nilipochukuliwa

Mwambie!

 

Mwambie na mwelekeo,  ule wa kutarikiwa

Alochukuwa macheo, wazimu mimi nikawa

Na lipofika machweo, kubadili kutokuwa

Mwambie!

 

Mwambie kwalo komeo, moyo ulivyochukiwa

Na chuki ilivyo leo, nimekubali fanyiwa

Kiwe kikali kinyweo, bado maji yatanywewa

Mwambie!

 

Mwambie cha matokeo,  kile kilikataliwa

Ndicho chanipa chocheo,  hatua kuegemewa

Kwani kuna marejeo, kurudi yasiyojuwa

Mwambie!

 

 

By The Mount Kenya Times

We are The Mount Kenya Times. For customer care, 📨 info@mountkenyatimes.co.ke or 📞 +254700161866 For feedback to editorial, 📨 news@mountkenyatimes.co.ke or 📞 +254705215262 or WhatsApp +254714090155

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *