Alfred Lobawoi
Wewe usiyenitaka, kuniona hadharani,
Kisa chuki umeweka, wanidharuliani?
Mimi nisiye na shaka, nina zangu hamkani,
Mwenye roho ya korosho, je unafaidi nini?
Wewe mvimbisha kichwa, ninazungumza nawe,
Acha kujifanya mchwa, kuniona mimi jiwe,
Unadhani nimeachwa, sababu siendi nawe?
Mwenye roho ya korosho, je unafaidi nini?
Wewe wajifanya bubu, nia yako iko wazi,
Kweli ulinighilibu, ndipo ukapande ngazi,
Sasa utapata tabu, kama ndiyo yako kazi,
Mwenye roho ya korosho, je unafaidi nini?
Wewe hata huna haya, unachofanya si sawa,
Ndiyo ya kwako tabiya, tangu ulipozaliwa,
Kizuri kwako kibaya, husiti kukichukuwa,
Mwenye roho ya korosho, je unafaidi nini?
Mtunzi: Alfred Lobawoi
Mahali: Ruiru
Similar Posts by The Mt Kenya Times:
- Mt Kenya Times ePAPER August 13, 2026
- The deputy’s dilemma: Gachagua warns Kindiki he is next
- KEMSA chief outlines supply chain reforms ahead of health summit
- Why Audi’s smaller models are often more desirable than their bigger brothers
- The politics of tomorrow: Why Kenya keeps replacing the future with the next election