Nakuaga nimetua, Agosti tutaonana,
Menifunza kufikia, malengo zilizofana,
Kujituma natilia, kunapokucha manana,
Ahsante semia, muhuri nimeiweka,.
Muhuri nimeiweka, sitaki tena uzembe,
Kini bado sijafika, nameza bado tembe,
Nilidhani utotuka, meisha haraka kumbe,
Ahsante semia, nakuvulia chepeo.
Nakuvulia chepeo, japo nimeinama
Mara nyingi sitakao, najikuta nimesimama,
Nikikumbuka walao, najipea moyo wima,
Ahsante semia, naridhikia kijeshi.
Naridhikia kijeshi, nitawamisi wenzangu,
Kumbukumbu za ucheshi, tulizozianza tangu,
Saizi nawashawishi, vikielea ni vyangu,
Ahsante semia, nitarudi niwezeke.
Nitarudi niwezeke, kwani wema hauozi,
Niko nahisi upweke, wacha nitafute kazi,
Tukirudi unizike, nitakubali tetezi,
Ahsante semia, tuonane Agosti.
Mtunzi: Malenga Mugo Romeo
Lakabu: Morio
Chuo Kikuu cha Murang’a