Tahakiki Ya Ndoto Ya Amerika Na Hayati Ken Walibora

Kitabu; Ndoto ya Amerika

Mchapishaji: Sasa Sema

Kurasa: 52

Mhakiki; Winjoy Gacheri

Ndoto ya Amerika ni nakala iliyoandikwa na Hayati ken walibora ambayo ni Nakala ya kusisimua na yenye mafunzo chungu nzima.Nakala hii inawahusika wafuatao Isaya yano(isa) ,mamake isa,madoa mamake Madoa,Rock mwamba,Mzee zakayo wekesa ,Mwalimu njoroge,Askari na wengine ambao sijataja.

Ndoto ya Amerika ni kitabu ambacho usichoweza kukiweka chini Hadi umeisoma hadithi nzima.Kitabu hiki kinawasisimua wasomaji wenye umri ndogo na mkubwa ambapo kimejaa mafunzo chungu nzima.

Ndoto ya Amerika ni Moja ya kazi maarufu ya mwandishi ken walibora ambaye ni maarufu Kwa uandishi wa hadithi zenye uzito wa kijanii hasa masuala ibuka .Katikati kitabu hiki chenye mada ndoto ya Amerika walibora anachambua maisha ya wahusika mbalimbali katika muktadha wa maisha ya kisasa ya kiafrika akilenga hasa mabadiliko ya kijamii

Ndoto ya Amerika inachunguza dhana ya ndoto katika jamii za kiafrika tukiangazia wahuasika Isa na Madoa ambapo wahusika Hawa wanatafuta maisha Bora uhuru na nafasi Yao kutambua ulimwenguni wa kisasa ikijumuishwa mbinu ya hadithi na Taswira zenye nguvu kuwasiliaha hisia za kutafuta na kutokuwa na uhakika

Wahusika katika Ndoto ya Amerika wanaonyeshwa kama watu wa kawaida lakini Wana ndoto kubwa.Walibora anawasilisha maisha Yao ya Kila siku changamoto wanazokabliana nazo na matamanio Yao hivyo kuwa Fanya wasomaji wawezw kuungana nao Kwa urahisi

Tunapata katika hikiitabi kuwa mamake isa alikua anakuza mazao mbalimbali kama vile mahidi maharagwe mtama mawele na mboga kisha akawauzia watu katika soko la sangura tunapata kuwa Isa alikua akichapwa viboko alipokataa kumsaidia kulima shamba lao ndiposa akachukia nyumbani ata zaidi anendelea kusema kuwa alichukua shule alifurahia tu wakati wa likizo au siku kuu za kitaifa Kwa maana hatakuwa na masomo.Unapata pia Mhusika Madoa alichukua kwao alikua akiishi na mamake ambapo alikua akiuza madazi chapati na sambusa katika soko la sangura.Tunaoata kuwa Madoa hakupenda masomo kwani hata hakuwa hakihudhulia masomo kila siku hakuwa anaelewa Chochote

Hayati ken walibora tunapata pia mtindo qa uandishi wake ni  wa kipekee sana ukijumuhisha matumizi ya lugha ya kuvutia na Taswira za kina.Anatumia lugha ya kiswahili Kwa ustafi mkubwa akichangamsha watu wa kiafrika na mitindo ya kisasa ya uandishi tunapata wahusika wawili wanapozungumza Madoa anasema kuwa nikifika huko Nitaitwa Michael Monday au Michael badala ya jina lake Madoa.Mwenzake anatueleza kuwa jina lake walimjua kama namasake Madoa aliahangaa sababu yake kupenda kubadiliaha jina

Ujumbe wa kitabu Cha ndoto ya Amerika ni mzito ukihusisha masuala ya utawala,ndoto za maisha Bora na kadhalika.walibora anatoa mwito Kwa jamii kuangalia Kwa makini malengo Yao na jinsi wanavyoweza kuyafikia tunapata kuwa ndoto ya wahusika Isa na Madoa ilikatika walipoenda kumtembelea rafiki ya Madoa rock mwamba ambaye tunaambiwa alikua jambazi hatari tunapata kuwa alipatikana na bunduki kumi na nane risasi arobaini na vitambulisho bandia kumi kinyume Cha Sheria pia alikuwa alijaribu kuiba Kwa kutumia nguvu katika nyumba moja kwenye mtaa wa buruburu na zaidi tunaambiwa kuwa aliwateka nyara watoto Saba na kuwaua pamaoja na kutoroka gerezani la kamiti.Isa alikua amekanywa mara kadhaa na mamake mzazi kutembea na Madoa ila hakumsikia tunapata kuwa mamake mzazi alimchapa Kila mara akijihusisha na madoa.Pia alikanywa kujihusisha na watu wenye tabia mbaya ila walitia maskio Yao nta ambapo Sasa wameiahia kufungwa gerezani isipokuwa  isa ambaye ripoti yake ilikua zuri

Kwa hitimisho ndoto ya Amerika ni kazi ya kusisimua na ya kufikiriaha ambayo inatoa mwanga na Hali halisi ya maisha katika jamii A kiafrika Kwa mtindo wake wa kipekee na unumbe wa kina katika hiki kitabu kinabaki kuwa chombo muhimu katika uandishi wa Taswira halisi ya ndoto na changamoto zinazowakabiliwa na watu wa kawaida ni kazi inayopaswa kusomwa na yeyote anayetaka kuelewa changamoto kijamii na kisiasa katika ulimwengu huu

 

By Wanjohi P. Mugambi

Wanjohi. P. Mugambi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *