Anwani: Utando Wa Ushairi
Wahariri: Derick Masika na Lilian Alivizda
Mchapishaji: Williams Publishers
Kurasa: 168
Mhakiki: Alfred Lobawoi
Kitabu hiki ni diwani ya mashairi yaliyotungwa kwa lugha ya Kiswahili. Kazi hii ambayo ni ya kurasa 168 imekusudiwa kwa wanafunzi wa kitembo cha shule ya upili pamoja na wapenzi wote wa fasihi. Haya ni kutokana na lugha iliyotumika kufinyanga mashairi na kutoa maelezo faafu ili kuwaandaa watahiniwa wa mitihani ya kitaifa na hata kuwaandalia jukwaa la kuwakuza kiutunzi.
Watunzi wa diwani hii wametumia vigezo viwili muhimu vya kutambua mashairi ili kumpa msomaji mwanga, navyo ni Mashairi Huru na Mashairi ya Arudhi. Isitoshe, mambo kama vile sifa za mashairi, muundo wa mashairi, istilahi mbalimbali zinazotumika katika ushairi kama vile mishororo, vina, bahari za mashairi vyote hivyo vimeangaziwa; ni nini pamoja na mifano ya kuonyesha umuhimu wake shairini. Pia viambajengo ambavyo hujitokeza wazi shairini vimegusiwa, mfano: Taswira (Oni, sikivu, mguso) na Matumizi ya lugha (Tashbihi, methali, tashihisi) havijasazwa.
Katika Uzi uo huo, mashairi mengi yaliyotungwa kwenye diwani hii yamejikita kuangazia maudhui ya kila nui. Si elimu, si mazingira, si anasa, si ndoa, si umasikini kwa kifupi itampa msomaji fursa ya kujifunza mambo mengi yaliyojikita katika maudhui hayo. Hayo yanaonyesha jinsi washairi walivyo na uwelewa kutokana na maeneo watokako na kutagusana kwao na kila kionjo cha maisha. Si hayo tu, ujuzi wao wa kutumia Uhuru wa kishairi umetawala kuwasaidia kupitisha ujumbe kishairi na kukidhi mahitaji ya kiarudhi.
Kilichonifurahisha katika kazi hii ni jinsi usawa ulivyopewa kipaumbele. Jambo jingine ni jinsi waandishi chipukizi walivyochangamkia mashairi kwa kujisabilia kwa ari na ilhamu na kulete sura mpya ambayo haijawahi kuwepo katika karne hii. Eneo walikotoka watunzi hawa kutawachochea sana waandishi na watunzi wengine kuanza kujifunza bila woga na kujiamini zaidi.
Ingawa diwani hii imefanikiwa kutekeleza haja kwa msomaji, bado ninahisi kuwa marekebisho kama vile ya upangaji maudhui yangefanyika basi ingekuwa heri zaidi. Marekebisho hayo yatakuwa ya manufaa makubwa kwa msomaji ili kutoa maelekezo ya kujua lipi linafaa kuwa wapi na kwa nini?
Yote hayo ni tisa, kumi ni kwamba kazi hii ni ya kupigiwa mfano. Hii ni tunu kwa msomaji yeyote yule mwenye mapenzi ya dhati ya kujifunza ushairi na lugha ya Kiswahili. Bahari tofauti ya mashairi yametungwa na washairi takriban 14 tena yenye lugha ya mnato. Ni matumaini yangu kuwa hata wale ambao walikuwa na dhana ya ushairi kuwa no mgumu watachochewa na muundo wa diwani hii aula na kuchovya asali watakavyo.
Similar Posts by The Mt Kenya Times:
- Clashes and arrests taint PSG’s Champions League triumph — 416 detained
- New group of western deportees arrives in Ghana from United States
- Defending Champion Coco Gauff Eliminated from French Open by Anastasia Potapova
- Reprieve for over 200 MKU students as Court quashes CS order to stop Oral Health degrees
- Kamuri calls for unity, safety amid market fire, school tragedy and Ebola facility debate