By Alfred Lobawoi
@themtkenyatimes

Worth Noting
“Malumbano baina yetu na washairi wakongwe, Mimi nilikua upande mmoja na mshairi Issa Amir Kilimo. Tulipendana sana na wezee tukiwaambia fani wawaachie vijana kwani hakuna njia njema walizotengeneza katika zama zao. Hiki kisa kilikua hatari sana, kilifanya gazeti la Tabibu lipate umaarufu mkubwa.
Ingawa watu wengi walinitazama kama mshairi mchanga hivyo basi walijua sito muweza Mwinyi Avuma au Farisi wa tungu, Mambo yalikuwa kinyume na matarajio ya wengi. Niliendeshana naya mpaka akaamua kukaa kimya. Jina langu likainuka sana.
Ushairi kupewa thamani ndogo. Kwangu hili naliona ndilo limeziba kila kitu hata leo hii ushairi umekuwa si chanzo cha mapato.
Viongozi wa serikali wapaze sauti na kuutumia ushairi katika matukio yao. Vyombo vya habari pia vitoe nafasi kwa ushairi kama kuweka vipindi vya ushairi redioni, kuweka kurasa magazetini ambapo watunzi watatuma mashairi yao, kisha mwisho kabisa ni Wafanya biashara wautumie ushairi kufanya matangazo ya biashara zao.”
Tueleze kwa kifupi Hamisi Kisamvu ni nani?
Hamisi Kisamvu ni mtoto wa Nne wa marehemu Ally Selemani Kisamvu aliyekua mshairi nguli katika zama zake miaka ya 1960 – 2002.
Msukumo wa kutunga mashairi niliupata toka kwa marehemu Mzee wangu, Nilikuwa nikimsikiliza akighani, na aliweza kunisimulia visa lukuki, ambavyo vilinipa hamasa ya kuwa mshairi.
Mazingira yako yalikuchochea vipi katika safari yako ya utunzi?
Mazingira yangu pia yalinipa hamasa kwa sababu nilikuwa naishi na kaka yangu ambaye alinitangulia kuwa mshairi. Mashairi yake yalikuwa yanachapishwa na kusikilizwa magezetini na redioni.
Ni matukio yapi ambayo unayakumbuka katika safari ya utunzi wako?
Matukio mengi sana lakini kuna moja nalikumbuka sana maana llichangia sana kunipandisha katika safari yangu ya utunzi. Ya kwanza, yalikuwa ni malumbano baina yetu na washairi wakongwe, Mimi nilikua upande mmoja na mshairi Issa Amir Kilimo. Tulipendana sana na wezee tukiwaambia fani wawaachie vijana kwani hakuna njia njema walizotengeneza katika zama zao. Hiki kisa kilikua hatari sana, kilifanya gazeti la Tabibu lipate umaarufu mkubwa. Wazee waliamua kutupuuza baada ya kuona ujana ndiyo unaotusumbua. Nakumbuka kuna mshairi mmoja yeye alikuwa upande wa wazee aliamua yeye kukivalia njuga hiki kisa, Huyu alikuwa mwanafunzi wa marehemu Andanenga ingawa watu wengi walinitazama kama mshairi mchanga hivyo basi walijua sito muweza Mwinyi Avuma au Farisi wa tungu, Mambo yalikuwa kinyume na matarajio ya wengi. Niliendeshana naya mpaka akaamua kukaa kimya. Jina langu likainuka sana.
Unapata faida ipi ukiwa mtunzi wa Mashairi?
Faida kubwa amabayo kwa sasa nimeipata kupita ushairi ni kadha, Mosi ni heshima ambapo naheshimika sana na ninamshukuru Mungu kwa hilo. Jambo la pili ni kuwa angalau nimeweza kufahamiana na watu wengi mno ndani na nje ya nchi yangu. Nalo ni shukurani kwake.
Ni changamoto zipi ambazo umekumbana nazo katika utunzi wako?
Changamoto ni nyingi lakini kubwa ni ushairi kupewa thamani ndogo. Kwangu hili naliona ndilo limeziba kila kitu hata leo hii ushairi umekuwa si chanzo cha mapato.
Unawapa ushauri upi Washairi Chipukizi?
Ushauri wangu kwa washairi vijana wanaoupenda na kutaka kuuenzi ushairi huu wa Kiswahili lazima wakubali kwenda kupiga goti na kujifunza kwa washairi wakongwe na mambuji, kinyume chake tungo watakua wanazivua nguo. Ushairi si tu vina na mizani,
Kwanza lazima tuseme, pili ni lazima tuinuke kuuhami ushairi huu maana kuna magaidi hawataki kuona ukitamba. Viongozi wa serikali wapaze sauti na kuutumia ushairi katika matukio yao. Vyombo vya habari pia vitoe nafasi kwa ushairi kama kuweka vipindi vya ushairi redioni, kuweka kurasa magazetini ambapo watunzi watatuma mashairi yao, kisha mwisho kabisa ni Wafanya biashara wautumie ushairi kufanya matangazo ya biashara zao.
Unahisi kama kuna utofauti kati ya Mashairi Huru na ya Arudhi?
Mimi naamni kuwa jambo lolote lenye taratibu sheria na kanuni ndilo jambo la kufuata, usahairi huu wa Kiswahili unavyo vyote hivi nauwacheje kwa mfano, Jambo la kwanza, Ushairi huu wa kimapokeo ndiyo wenye ujuzi, maarifa na mbinu siyo kama huo mwingine. Hao wengine wanasema ushairi huu unamfunga mtunzi ila si kweli, hao ni sawa na mtu aliyeshindwa kupika akasingizia moshi. Huku kuna uhuru wa mshairi wa kufanya atakavyo bila kuacha arudhi, kuna inkisari, mazida kuboronga sarufi ; vyote hivi vinakupa uwezo wa kuandika utakavyo.
Anayetaka kufaidi kupitia kazi zako atazipataje?
Kwa wale wanopenda kusoma kazi zangu unaweza kuagiza diwani zangu. Nimeandaa diwani kadha wa kadha; Diwani ya Mkanyaji , Mwenda Kizani, Siwa ya Msimaozi, Tunu ya taifa, Kijaluba cha Nudhumu. Na diwani mpya kabisa ya utenzi ; Tenzi za Mausi Mema
+2550)715311590/062291816
Email: kissmvujr@gmail.com
Face book Hamis kisamvu mkanyaji

