
Kitabu: Siku Njema
Mchapishaji: Longhorn Publishers
Kurasa: 80
Mhakiki : Winjoy Gacheri
Siku njema ni Riwaya iliyoandikwa na Hayati ken walibora.Riwaya hii Ina wahusika kadhaa.Baadhi Yao ni zainabu mukame,Mwinyimsa mukame ,kitwana,Athman Ali,Rehema,Rahma na wengine wengi ambao sijataja
Ningependekeza kitabu hiki Kwa wale wanaopeda hadithi zenye mafunzo na wanataka kujifunza zaidi kuhusu thamani ya maisha na ushirikiano na wengine.Siku njema ni Riwaya iliyojaa mafunzo chungu nzima
Siku njema ni Riwaya inayoshughulia masuala ya maisha ya Kila siku na changamoto zinazokabili jamii.Katika hadithi hii mwandishi anatueleza maisha ya wahusika wakuu wakionyesha matukio ya furaha,huzuni,na matumaini.Mwadishi anatuambia kwamba mamake alipozaliwa babu yake mwinyimsa makame alikua amebugia chumvi ya kutosha.Anasema kuwa alikua katambaliwa pakubwa na ukongwe .Day lake shaibu yule lilikua karibu kutia nanga ufuoni baada ya safari ya miaka Mingi katika bahati ya maisha.Anaendelea kusema na punde baada ya siku chache mzee makame alikufa.mamake akiwa bado kichanga.Anasema kwamba baada ya kifo cha Babu mji wake ulikumbwa na magumu yasiyo na kifami.Uhaba wa chakula na nguo ukashamiri vilivyo.Tunapata pia wakewenza hao na wana wao walipigana na kuchanian hadharani bila haya .usihiri ulikua umeingia na kukita mizizi mchangani kiasi cha kuwa mwandishi anasema kwa babu yake palikua hapa kaliki
Mwandishi natumia hadithi hii kuonyesha umuhimu wa matumaini na jinsi mtu anavyoweza kushinda vikwanzo vilivyopo kwenye maisha.Ujumbe wa kuendelea kutafuta furaha unajitokeza wazi katika matendo ya wahusika .mwandishi anasema kuwa anakumbuka selemani mapunxa vizuri sana waliokuwa wanaketi naye dawati Moja.Anasema selemani alikua kisu kilichosenea hakifui dafu hata vibaya vibaya anasema kuwa alizoea Kwa jicho la upembe ili aone ameandika Nini katika mtihani na tamrini aweze kuandika vivyo hivyo.Wakati wa mtihani alinyenyekea na kujifanyia rafiki yangu wa dhati lakini siku nyingine mwandishi asema kuwa alikua anamzonea na kumwita mwanaharamh MSI baba Kwa adili na Kani kuwashunda wanafunzi wengine wote palikua na fununu kuwa alikua ameenda mpaka Kwa mganga kuagua Nini kilichomfanya asiwe hodari na tunajuzwa kuwa ilisemeka ni Mimi ndiye nilyemkosesha bahati yake.Binamu zake ata alipokua akichekwa anasema pia wao walikua mstari wa kwanza kumcheka isipokuwa vumilia tu ndiye aliyekua akimtetea
Katika Riwaya hii ya siku njema wahusika ni wa kina na wanawakilisha tabaka tofauti za jamii.kila mmoja ana hadithi yake na kupitia wao.tunapata mtanzamo wa kina kuhusu maisha Yao na changamoto wanazokabiliana nazo.uhusiano Kati ya wahusika unatoa mwanga juu ya umuhimu wa ushirikiano na mshikamano katika jamii.
Mhusika mmoja Kwa jina mwanadamu anamwambia mjomba wake kuwa waliopofiwa na babayao wakiwa bado wadogo walipata tabu ambazo hazina kifani.Anasema aliona atabaki maskini Sina Sinani nikiulizwa siungami.Ansema kuwa alijitahidi Hadi hii Leo anaweza kujikidhia hitaji lake
Pia mwandishi wa Riwaya hii anatumia lugha rahisi na ya kueleweka ambayo Inafanya hadithi iweze kufikiwa na wasomaji wa Kila umri Kwa urahisi.Mtindo wa uandishi ni wa kuvutia ukiwa na Taswira nzuri na maelezo yanayochora picha wazi katika akili ya msomaji.Mwandishi anasema kuwa akitaka Aishi mbali na kina amina Aishi maisha yake mwenyewe aumane na ulimwengu mwenyewe.
Kwa kifupi siku njema ni Riwaya iliyohamasisha na inatufundisha kwamba licha ya changamoto za maisha daima Kuna nafasi ya matumaini na furaha.Ni kitabu ambacho kinapaswa kusomwa na Kila mtu anayetafuta kuelewa zaidi kuhusu maisha na umuhimu wa kushikamana na wengine